TAZAMA yatoa Gawio la Bilioni 4.35 baada ya kupita miaka 15


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amepokea gawio la Serikali la zaidi ya Shilingi Bilioni 4.35, kutoka Kampuni ya Bomba la Kusafirisha Mafuta la Tanzania - Zambia (TAZAMA).

Bw. Mchechu amesema utolewaji wa gawio hilo unaakisi moja kwa moja falsafa za R4 za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za Maridhiano, Ustahimilivu, Mabadiliko na Kujenga upya.

Mchechu amesema hayo katika hafla ya utoaji wa gawio hilo iliyofanyika leo Agosti 26,2024 Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko aliyekuwa mgeni rasmi.

Umri huo kama mtumishi wa umma amebakiza miaka miwili kustaafu, anakuwa kidogo mnyonge mnyonge lakini kwa Tazama badala ya kuwa mnyonge ndio imekuja juu, imekuwa tofauti kidogo, alisema Mchechu. 

"Kinachofanyika leo kimetutia faraja kubwa sana, Shirika la TAZAMA lilianza miaka 58 iliyopita katika miaka miaka hiyo ingekuwa ni umri wa mtu anakuwa na miaka miwiili kabla hajastaafu, lakini Tazama imeanza kuamka na nguvu kubwa ikiwa na miaka hiyo 58” amesema Mchechu.

Akifafanua zaidi amesema kuwa Shirika hilo ukiaacha kile kipindi cha mwaka 2019 wana miaka 15 ambayo wana hisa hawajapata Gawio, lakini katika mababadiliko ambayo yanasimamiwa nanchi hizo mbili na viongozi wake na kwa upande wetu Tanzania mageuzi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Makatibu wakuu wake katika utekelezaji wameona  manufaa yake na hivyo anamshukuru Mhe. Rais namna ambavyo wametekeleza na kuziishi hizi 4R kwa kiwango cha juu.

Aidha, ameipongeza TAZAMA, na kusema kwamba faida waliyoanza nayo sio tu wameizalisha kwa mwaka mmoja, lakini ni faida ambayo ni kubwa kwa mpigo katika kipindi cha mwaka mmoja ambao hawajawahi kuzalisha lakini wamepata faida ya Sh. Bilioni 52.25, kwa hiyo wameanza kwa kishindo na kishindo chao ni kikuu kimesikika.

“Mheshimwa Waziri Mkuu, gawio kama hili ambalo tumepata leo tunawashukuru sana TAZAMA, nakama ulivyoelekeza fedha hizo ziende kwenye miradi ninasema itakwenda, na nafikiri tutaendelea kupata gawio kubwa zaid,” amesema Mchechu.

Amesisitiza Kiwango kilichopatikana cha Bilioni 4.35 ni kikubwa kwa taasisi ambayo ilikuwa inasuasua.

Pamoja na Mambo mengine Mchechu a,etumia fursa hiyo kwa kuwapongeza TAZAMA kwa hatua hii waliyofikia, na kuwahimiza  kuendeleza juhudi waizozianzisha ili mwaka ujao wafanye vizuri zaidi.


Chapisha Maoni

0 Maoni