SGR yazidi kunoga, TRC yaongeza safari za treni

 

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza mabadiliko ya ratiba na ongezeko la safari za treni za reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) kati ya Dar es Salaam na Morogoro kuanzia Julai 5, 2024.

Taarifa iliyotolewa leo Julai mosi, na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Jamila Mbarouk, imesema ongezeko la safari litahusisha kuanza kwa treni mpya ya haraka (express train).

Jamila Mbarouk amesema kwenye taarifa hiyo kuwa treni hiyo mpya ya haraka itakuwa ikifanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Morogoro bila ya kusimama vituo vya kati.

Treni ya haraka itakuwa ikiondoka Dar es Salaam 12:00 asubuhi na saa 1:10 usiku na itaondoka Morogoro 12:30 asubuhi na saa 1:30 usiku, imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema treni ta kawaida ya SGR itaondoka Dar es Salaam 3:30 asubuhi na saa 10:00 jioni na itaondoka Morogoro saa 3:50 asubuhi na saa 10:20 jioni.

Taarifa hiyo imemalizia kwa kusema kwamba Shirika la Reli Tanzania (TRC) litaendelea kuongeza safari kulingana na ongezeko la idadi ya abiria ili kutoa huduma bora na za uhakika.

Chapisha Maoni

0 Maoni