Manji kuzikwa leo huko Florida nchini Marekani

 

Mfanyabiashara maarufu Tanzania Bilionea Yusuf Manji ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti na Mfadhili wa Klabu ya Yanga, anatarajiwa kuzikwa leo huko Florida nchini Marekani.

Manji alifariki dunia jumamosi usiku katika hospitali ya Florida, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na mtoto wake Mehbub Manji.

Mehbub amewashukuru watu mbalimbali wakiwamo Watanzania ambao wameendelea kuomboleza kifo cha baba yao, na kuwashukuru kwa maombi yao.

Chapisha Maoni

0 Maoni