Mambo si shwari baina ya Rais Ruto na Naibu Rais wake

 

Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua ameonesha dalili ya kuwa mambo si shwari baina yake na Rais William Ruto.

Hata hivyo, Gachagua amesema masuala yanayowakwamisha katika uhusiano wake na Rais Ruto, yanazungumzika katika moyo wa kuimairisha maendeleo, umoja na demokrasia.

Amesema mgawanyiko serikali ya Kenya Kwanza, unachochewa na watu waliojiunga na serikali hivi karibuni, ambao ndio wanaamua namna wale waliokuwa na Rais Ruto katika nyakati nzuri na mbaya wanawezea kushirikiana na rais.

Kwa mujibu wa gazeti la Nation la Kenya, kama hiyo haitoshi katika kuonyesha mgawanyiko Gachagua atafanya mdahalo wake pekee na kundi la vijana wa Gen Z, kuhusu masuala ya utawala wa serikali, nje na ule ulioandaliwa na Rais Ruto.

Chapisha Maoni

0 Maoni