Makamu wa Rais wa Marekani Bi. Kamala Harris amepata kuungwa mkono na idadi ya kutosha ya wajumbe wa Democratic kuwa mgombea urais wa chama hicho.
Utafiti uliofanywa na Associated Press, jumatatu umesema Bi. Harris anaungwa mkono na zaidi ya wajumbe 1,976 idadi ambayo inatosha kushinda hatua ya kwanza ya kura za uteuzi.
Kwa upande wake Bi. Harris amesema anajivunia kupata kuungwa mkono kwa kiasi kikubwa na anatarajia kuridhia rasmi uteuzi wake.
Wajumbe ni watu waliochaguliwa kuwakilisha maeneo yao ya uchaguzi kwa ajili ya kuwakilisha maeneo hayo katika Mkutano wa Kitaifa wa chama cha Democratic wa kuteua mgombea.
Makamu wa Rais wa Marekani Bi. Kamala Harris inaaminika kuwa ni anauwezo wa kumshinda mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump.
0 Maoni