Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda
ametembelea meli ya matibabu ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona
matibabu yanavyofanyika.
Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa
Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ.
Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia
nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi
ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na
Jeshi la Ukombozi la Watu wa China.
Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi leo tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini kesho tarehe 23 Julai mwaka huu.
0 Maoni