Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema mikopo ni moja ya vyanzo vya mapato ya serikali kote duniani, hivyo Tanzania kukopa sio aibu wala kujidhalilisha, bali ni sifa njema kwa kuwa inakopesheka.
Simbachawene ametoa kauli wakati akizungumza kwenye harambee
ya kuchangia fedha kwa ajili ya kubadilisha paa la Kanisa Katoliki Parokia ya
Mtakatifu,Yuda Tadei Mang'ola Chini,
Wilaya ya Karatu, Mkoani Arusha, ambalo limekuwa likivuja wakati wa mvua na hivyo kusababisha wakristo kushindwa kukaa
ndani.
Amesema vyanzo vya mapato vya Kanisa ni pamoja na sadaka ya kila jumapili, zaka,
misaada mbalimbali pamoja na harambee
huku akitaja vyanzo vya mapato
vya Serikali kuwa ni kodi, tozo, misaada
na mkopo, na kusema kukopa ni moja ya
chanzo cha mapato ya serikali na serikali zote duniani zinakopa.
Aidha, amesema kama ingetokea Tanzania haiwezi kukopesheka
hiyo ndo ingekuwa aibu lakini kwa kuwa
inakopsheka hiyo ni heshima kubwa kwa watanzania kwa kuwa inakopa ili
kutekeleza miradi ya maendeleo na kama
isipofanya hivyo itapelekea nchi kupata
madhara makubwa ambayo yasingetokea kama ingekopa.
Amesema Nchi zote duniani ikiwemo Marekani na China zinakopa na
zinadaiwa na kwamba kodi inayokusanywa nchini haina uwezo wa kutekeleza
miradi hiyo na kama kodi hiyo itaweza kutumika inaweza kuchukua zaidi ya miaka
40 ili kukamilisha miradi hiyo.
"Vyanzo vya mapato vya Kanisa ni sadaka ya kila
jumapili, zaka, misaada mbalimbali pamoja na harambee ambapo harambee ni hatua ya
mwisho ya utafutaji wa fedha kwa Taasisi za dini, lakini vyanzo vya mapato vya
Serikali ni kodi, tozo, misaada na
mkopo, hivyo kukopa ni moja ya chanzo cha mapato ya serikali na serikali zote
duniani zinakopa," amesema Simbachawene na kuongeza kuwa,
"Kukopa ni
chanzo cha mapato hivyo isionekane Serikali ya Chama cha Mapinduzi inayoongozwa
na Rais Samia Suluhu Hassan inapokwenda kutafuta mkopo kwa ajili ya kutekeleza
miradi ya kimkakati ya maendeleo ndo
inakopa sana,"
Amesema kutokana na mahitaji makubwa ya nchi suala la kukopa
haliepukiki akitolea mfano uendelezaji wa Bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu
Julius Nyerere ambalo gharama yake ni zaidi ya
trioni 6 huku bajeti ya Serikali
ya mwaka mzima ikiwa ni tirioni 43 huku zaidi ya asilimia 7O ya fedha
hizo zikitumika kwa ajili ya uendeshaji wa nchi na asilimia 30 ndizo hupelekwa
kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.
"Hivi tungetaka kujenga reli ya SGR kwa kodi yetu tungejenga kwa miaka mingapi?amehoji Simbachawene na kusema ikijengwa kwa miaka 100 itakuwa na tija kweli na tukiamua
tutaweza kujenga kwa miaka 50 au 60
ambapo hapo tutaacha kulipana mishahara,
kusomesha watoto pamoja na kutibu
wagonjwa. "
Amesema "Mbali na utekelezaji wa miradi hiyo ya kimkakati,
Serikali chini Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea na ujenzi wa madarasa ambayo
ili kumaliza upungufu wa madarasa uliopo sasa kama zisipokopwa changamoto hiyo itatuliwa ndani ya kipindi
cha zaidi ya miaka 25 ijayo huku idadi
ya watu ikizidi kuongezeka."
"Unataka Rais
Samia akae tu asiende kukopa" amehoji Simbachawene na kususitiza kuwa,
"Kukopa ni chanzo cha mapato na
kukopa sio kujidhalilisha, Tanzania ina
sifa hiyo ya kukopa. Nchi
inayoweza kukopesheka ni nchi yenye heshima
kama ilivyo Tanzania kwani
mashirika makubwa ya fedha duniani ikiwemo Benki ya Dunia na Shirika la fedha
Duniani ( IMF) zimeweka vigezo za vya kuweza kukopesheka na Tanzania inakopesheka kwa sababu ina vigezo."
Hata hivyo Mhe. Simbachawene amesema kwa mujibu wa kanuni za
fedha duniani zinaipa Tanzania wigo wa ukomo wa kukopa na kama nchi bado ina
sifa ya kukopa kwa sababu bado haijafikia kikomo hicho.
Amesema "Hivi reli ikishajengwa inarudia tena kujengwa
, umeme ukianza kuzalishwa tunarudia tena, viwanja vya ndege, madaraja,
madarasa na vituo vya afya vinavyojengwa nchi nzima havirudiwi tena kujengwa na
hivi ndo vinajenga uchumi kisha tunasonga mbele," amesema Simbachawene .
"Fedha hizi zinazokopwa ni muhimu kwa maendeleo ya nchi huku akitolea mfano Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Dodoma ndani ya kipindi cha miaka mitatu chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan haikuwahi kupata fedha nyingi za maendeleo ndani ya kipindi cha miaka 20 iliyopita."
0 Maoni