Aliyekuwa RC Simiyu ashikiliwa na polisi kwa kulawiti mwanafunzi

 

Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linamshikilia aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu Yahaya Ismail Nawanda mwenye umriwa miaka 46 anayedaiwa kumuingilia kinyume na maumbile mwanafunzi wa kike wa chuo kikuu Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Kamishna Msaidizi wa Polisi DCP Wilbroad Mutafungwa amesema tukio hilo limetokea tarehe mbili ya mwezi huu katika eneo la Klabu ya Rock City majira ya usiku.

Kamanda Mutafungwa amesema bado wanamuhoji mtuhumiwa huyo kwa kushirikiana na taasisi nyingine za kiuchunguzi na uchunguzi utakapokamilika mtuhumiwa huyo atafikishwa Mmahamani kujibu tuhuma zinazomkabili.


Chapisha Maoni

0 Maoni