Dkt. Ndugulile kuwania uongozi Shirika la Afya Duniani

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemchagua na kumpendekeza Dkt. Faustine Ndugulile kugombea nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika ambapo ni kwa mara ya kwanza Tanzania inatoa mgombea wa nafasi hiyo.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo jana wakati wa uzinduzi wa kampeni za kugombea nafasi hiyo aliyopendekezwa Dkt. Faustine Ndugulile mwenye uzoefu na ujuzi mkubwa katika masuala ya Afya Duniani ambae pia ni Daktari wa Taaluma hiyo.

“Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zinafanya vizuri sana duniani katika mapambano dhidi ya magonjwa ya kuambukiza, magonjwa yasiyoambukiza pamoja na kuimarisha huduma za afya ya uzazi mama na mtoto, Tanzania tumefanikiwa kupunguza vifo vya wanawake wajawazito kwa zaidi ya asilimia 80,″ amesema Waziri Ummy.

Chapisha Maoni

0 Maoni