Ramadhani Brothers wafikisha tuzo za AGT Serengeti

 

Wachezaji wa sarakasi nyota Ramadhani Brothers wamefikisha tuzo za America’s Got Talent katika hifadhi bora barani Afrika Serengeti baada ya kuzifikisha katika kilele cha Afrika, kilele cha Uhuru (Mita 5985) hifadhi ya Taifa Kilimanjaro.

Vijana hawa wanaendelea kutangaza utalii wa Tanzania ikiwa ni juhudi moja wapo za kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutangaza utalii wa duniani.

Washindi hao wa za America’s Got Talent, hivi karibuni pia walifanikiwa kukwea hadi kileleni mwa Mlima Kilimanjaro, wakiwa na tuzo hizo za @agt katika mwendelezo wa kuvitangaza vivutio vya utalii vya Tanzania.

TANAPA inakukumbusha kuendelea kupigia kura Hifadhi ya Taifa Serengeti na Mlima Kilimanjaro

𝗝𝗶𝗻𝘀𝗶 𝘆𝗮 𝗞𝘂𝗽𝗶𝗴𝗮 𝗞𝘂𝗿𝗮

Fungua tovuti ya

www.worldtravelawards.com/vote


Chapisha Maoni

0 Maoni