Rais Samia ahimiza mtaumizi ya nishati safi ya kupikia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Doto Mashaka Biteko mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuzindua Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia tarehe 08 Mei, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na viongozi mbalimbali wakati Wimbo wa Taifa ukiimbwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Mei, 2024.

Na Mwandishi Wetu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa kwa sasa inakadiriwa hekta 469,000 za misitu zinateketea kila mwaka nchini Tanzania, ikichangiwa kwa kiasi kikubwa na matumizi ya kuni na mkaa.

Mhe. Samia amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akizindua Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024/2034 unaolenga kupunguza matumizi kuni na mkaa katika kipindi cha miaka 10.

Amesema kutokana na ukataji wa misitu hiyo hata upatikanaji wa kuni na mkaa umeanza kupungua, jambo ambalo linapelekea wananchi kutumia muda mwingi kutafuta kuni na mkaa kuliko hata muda wanaotumia kutafuta chakula.

Amesema mbali na athari za mazingira, inakadiriwa kuwa Watanzania zaidi ya 33,000 hupoteza maisha kila mwaka kutokana na magonjwa ya kupumua ambayo kwa kiasi kikubwa huchangiwa na uvutaji wa moshi, kutokana na matumizi ya kuni ambao ni wanawake.

Chapisha Maoni

0 Maoni