NHIF yarejesha dawa 178 kwenye kitita kipya

 

Mfuko wa Bima ya Taifa (NHIF), umerejesha dawa 178 pamoja na kujumuisha dawa nne zilizokuwepo kwenye mwongozo wa Taifa wa matibabu lakini hazikuwemo kwenye Orodha ya Taifa ya Dawa Muhimu (NEMLIST) ambapo umezijumuisha dawa hizo kwenye Kitita chake cha Mafao cha Mwaka 2023.

Mfuko wa NHIF imeeleza hayo kupitia taarifa yake kwa umma iliyotolewa jana Dodoma, ambayo imeeleza kuwa hatua hiyo inaongeza wigo wa upatikanaji wa dawa kwa wanachama kwa kuzingatia miongozo ya tiba nchini.

Kutokana na maboresho hayo, Mfuko wa Taifa Bima ya Afya unawahakikishia wanachama wake kuwa huduma za matibabu zitaendelea kupatikana katika vituo vyote vilivyosajiliwa nchi nzima na endapo kutakuwa na changamoto za kiutekelezaji NHIF inashauri vituo viwasiliane nao.

Taarifa hiyo pia, imeeleza kuwa iwapo mwanachama atakutana na changamoto yoyote wakati wa kupatiwa huduma asisite kuwasiliana na Mfuko kupitia Kituo cha Huduma kwa Wateja, kwa kupiga simu bila malipo kwa namba 199.

Chapisha Maoni

0 Maoni