TANAPA yaandaa Futari na kutoa mkono wa Eid

 

Katika kuendeleza ukarimu kamaishara ya upendo kwa wadau na jamii kwa ujumla katika mwezi huu wa Ramadhani, Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) jana liliandaa futari ya pamoja iliyofanyika Makao Makuu ya TANAPA jijini, Arusha.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Kamishna wa Uhifadhi TANAPA- Musa Nassoro Kuji aliyeambatana na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Sheikh Shabaani Jumaa na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.

Tukio hili limewaleta pamoja wadau na watu wenye mahitaji maalum, ambao walipatiwa zawadi mbalimbali kwa ajili ya Sikukuu ya “Eid el Fitr” zawadi hizo zimekabidhiwa na Kamishna wa Uhifadhi TANAPA.

Kamishna wa Uhifadhi TANAPA- Musa Nassoro Kuji akisalimiana na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Sheikh Shabaani Jumaa, wakati akimkaribisha kwenye Futari iliyoandaliwa na TANAPA.


Wageni waalikwa wakipata Futari iliyoandaliwa na 
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) jana kwenye ofisi zake za Makao Makuu jijini Arusha.


Zawadi mbalimbali kwa ajili ya Sikukuu ya “Eid el Fitr” kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum
zilizokabidhiwa kwa wahitaji na Kamishna wa Uhifadhi TANAPA.

Chapisha Maoni

0 Maoni