Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini
(TARURA), Mhandisi Victor Seff amemtaka Mkandarasi ambaye ni China Henan
International Cooperation (CHICO) kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara za lami
za Mtili- Ifwagi (Km 14) na Wenda- Mgama (Km 19) zinazotekelezwa chini ya mradi
wa RISE mkoani Iringa.
Ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye ziara ya ukaguzi wa
mradi ili kujionea maendeleo ya mradi huo ambapo amemtaka mkandarasi huyo
kutimiza mkataba wake kama ulivyopangwa.
Mhandisi Seff amemtaka Mkandarasi CHICO kuongeza kasi zaidi
ili kumaliza kazi kwa muda uliopangwa wa mkataba ili wananchi waweze kutumia
barabara hizo katika kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wa nchi.
Wakati huohuo akiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi,
Mhandisi Seff alitembelea ujenzi wa barabara ya Sawala-Mkonge-Iyegeya (Km 10)
inayojengwa kwa kiwango cha lami kwa kutumia teknolojia mbadala (Ecoroads).
Mradi wa RISE una lengo la kuboresha barabara zenye fursa za
kiuchumi hasa maeneo yenye uzalishaji wa mazao ya kilimo na unatekelezwa katika
mikoa ya Iringa, Tanga, Geita na Lindi.
0 Maoni