Muhimbili yabadilisha damu kwa mgonjwa mwenye Selimundu

 

Hospitali ya Taifa Muhimbili imefanya huduma ya kubadilisha damu kwa mgonjwa wa Selimundu (Sickle Cell) na kuendelea kuwa hospitali inayoongoza katika kutoa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi hapa nchini.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Damu Muhimbili Dkt. Eunice Shija amesema huduma ya kubadilisha damu inafanyika kwa wagonjwa wenye Selimundu ambao wanachangamoto mbalimbali ikiwemo wenye changamoto ya kupumua na wale waliopooza.

Pamoja na hayo ameongeza kuwa huduma hiyo pia inatumika kuvuna mazalia ya damu ikiwemo chembe sahani au seli mama ambapo inaweza kutumika katika upandikizaji wa uloto pamoja na kubadilisha majimaji ya damu( plasma)  kwa ajili ya magonjwa mbalimbali ikiwemo shida ya kinga ya mwili.

Huduma ya kubadilisha damu na kuvuna mazao ya damu inafanyika kila siku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kuanzia Jumatatu hadi Jumapili kuanzia saa 2 : 00 Asubuhi hadi 11 : 00 Jioni 

Chapisha Maoni

0 Maoni