Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amewaalika wanawake
kushiriki katika Kongamano la Nishati Safi ya Kupikia linalotarajiwa kufanyika
katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Machi 9 Jijini Dodoma.
Kapinga amesema kuwa kongamano hilo linatarajiwa
kuwakutanisha wanawake zaidi ya 4000 kutoka Wilaya na Mikoa mbalimbali ambapo
pamoja na mambo mengine wanawake hao watapata fursa ya kujifunza kuhusu hatua
zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha nishati safi inapatikana kwa
kila Mtanzania.
Amesema pia Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa
nishati safi ya kupikia wanatarajiwa kugawa majiko ya gesi pamoja na majiko
banifu ikiwa ni muendelezo wa juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya
Awamu ya Sita chini ya Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha ifikapo mwaka
2033 zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.
0 Maoni