Watu wanane wafa baada ya kula kasa Pemba

 

Watu wanane wa familia sita tofauti wamefariki dunia na wengine 34 wanapatiwa matibabu Hospitali Kisiwa Panza, Mkoa wa kusini Pemba Visiwani Zanzibar baada ya kula samaki aina ya kasa.

Taarifa kutoka Pemba zinasema kwamba watu hao baada ya kula samaki huyo aina ya kasa hapo jana walianza kuumwa tumbo, kulegea mwili, kutapika na kuharisha.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mattar Zahor, amesema sampuli za matabishia na damu zimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kutambua kilichosababisha vifo hivyo.

Chapisha Maoni

0 Maoni