Wanawake OMR washiriki Kongamano la Nishati Safi

Watumishi Wanawake wa Ofisi ya Makamu wa Rais, leo Machi 9, 2024 wameungana na wanawake kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar katika Kongamano la Wanawake la Nishati Safi ya Kupikia linalokwenda sambamba na ugawaji wa mitaji na vitendea kazi vya Nishati safi ya kupikia kwa wajasiriamali mbalimbali nchini.

Lengo la kongamano hilo ni kuhamasisha jamii kuachana na matumizi ya nishati chafu ya kupikia itokanayo na matumizi ya kuni na mkaa kwa kumtua mwanamke kuni kichwani ili kuepukana na madhara mbalimbali ya  kiafya na uharibifu wa mazingira yatokanayo na matumizi makubwa ya nishati chafu ya kupikia isiyo salama na rafiki kwa mazingira. Inakaduriwa kuwa kufikia mwaka 2033/34 asilimia 80% ya Watanzania watakuwa wanatumia Nishati safi ya kupikia na hivyo kuhifadhi na kulinda mazingira kwa vizazi vya sasa na baadaye.

Kongamano hili linafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete (JKCC) jijini Dodoma ambapo Mgeni Rasmi 




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikagua jiko zinazotumia nishati ya gesi na umeme wakati akikagua mabanda ya maonesho katika Kongamano la Wanawake la Nishati Safi ya Kupikia linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma Tarehe 09 Machi 2024.


Chapisha Maoni

0 Maoni