Rais Dk. Mwinyi avipongeza vikosi vya JKU, Chuo cha Mafunzo na Zimamoto

 

Kamanda Mkuu wa Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amevipongeza Vikosi vya Jeshi la Kujenga Uchumi(JKU), Zimamoto na Uokozi na Chuo cha Mafunzo kwa ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa madarasa, masoko na vituo vya wajasiriamali.

Rais Dk. Mwinyi amesema hayo akizungumza na Maafisa na Wapiganaji alipowatembelea Vikosi vya Zimamoto na Uokozi, JKU na Chuo cha Mafunzo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea Vikosi vya SMZ tarehe: 9 Machi 2024.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi amehimiza umuhimu wa nidhamu, uzalendo, uadilifu na umoja kwa Maafisa na Wapiganaji hao.

Rais Dk. Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya vikosi hivyo.



Chapisha Maoni

0 Maoni