Mhe. Matiko aendelea kukusanya kero za Sekondari Mara

 

Katika kuhakikisha anafuatilia kwa karibu kero mbalimbali za wananchi zikiwemo za elimu  Mbunge Viti Maalumu katika Mkoa wa Mara, Mhe. Esther Matiko, amekuwa akizitembelea shule kadhaa kujionea mwenyewe kero mbalimbali.

Safari hii Mhe. Matiko amefika Shule ya Sekondari Tagota inayopatikana Halmashauri ya Mji wa Tarime na kuzungumza na walimu na wanafunzi wa shule hiyo, ili kusikia na kujionea kero zinazowakabili.

Huu ni mwendelezo wa Mhe. Matiko katika mpango wake wa ukusanyaji wa changamoto mbalimbali za kielimu kwenye mkoa huo katika kuelekea Bunge la Bajeti linalotarajiwa kuaanza vikao vyake mwezi wa nne 2024.



Chapisha Maoni

0 Maoni