CCM wampa pole Rais Dk. Mwinyi

 

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amepokea salamu za pole kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa Mhe.Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi akiongozana na wajumbe baadhi wa Sekretarieti ya Halmashauri ya Chama cha Mapinduzi Taifa waliofika  Ikulu Zanzibar jana.

Wajumbe hao  akiwemo Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar  Dkt. Mohamed Dimwa, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Paul Makonda, Katibu wa NEC Idara ya Organaizesheni Ndugu Issa Haji Ussi (Gavu), Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndugu Rabia Abdallah Hamid  kufuatia kifo cha Baba yake Mzazi, Mwenyekiti wa CCM Taifa Mstaafu, Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyefariki dunia tarehe: 29 Februari 2024, Dar es Salaam na kuzikwa tarehe: 02 Machi 2024, Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja.



Chapisha Maoni

0 Maoni