NEC kutangaza utaratibu wa kugawa majimbo

 

Bunge limeambiwa kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kutangaza utaratibu na sifa za kugawa majimbo mbalimbali nchini, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga amesema kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, NEC imepewa mamlaka ya kuchunguza mara kwa mara maeneo ili kugawa mipaka ya majimbo ya uchaguzi angalau kila baada ya miaka 10 baada ya kupata kibali kutoka kwa Rais.

Mhe. Nderianaga alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Nachingwea, Mhe. Amandus Chinguile aliyetaka kufahamu ni lini Serikali italigawa jimbo la hilo.

Mhe. Chinguile ameshauriwa kuwasilisha maombi ya kugawa jimbo hilo mara tu NEC itakapotangaza kugawa au kubadili majina ya majimbo ya uchaguzi.

Chapisha Maoni

0 Maoni