Mwili wa Lowassa wawasili KIA, msafara waelekea Monduli

 

Mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Ngoyai Lowassa umewasili leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), na kupokelewa na viongozi mbalimbali waliofika uwanjani hapo.

Mwili wa Lowassa umewasili KIA leo Februari 15, 2024 majira ya saa 5:22 asubuhi ukitokea Dar es Salaam na kupokelewa na waombolezaji waliwamo wakuu wa mikoa, Nurdni Babu, John Mongela na Waziri Kindamba wakiwa na Kamati ya Usalama.

Baada ya mwili wake kuwasili, msafara wa kwenda kijijini kwake Ngarash, Wilayani Monduli mkoani Arusha ulianza ukiwa na magari zaidi ya 100 likiwemo la Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lililoubebeba mwili huo.

Lowassa aliyefariki dunia Februari 10, 2024 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu, atazikwa jumamosi Februari 17, nyumbani kwao katika kijiji cha Ngarash.

Chapisha Maoni

0 Maoni