Mhe. Matiko mshindi wa tiketi ya ndege Qatar Airways Bunge Bonanza

 

Mapema leo asubuhi ndani ya ukumbi wa Bunge Spika wa Bunge la Tanzania Mhe Dkt Tulia Ackson amentangaza Mh Esther Nicholas Matiko kuwa mshindi wa jumla kwenye michezo ya Bunge Sport Bonanza 2024 lililofanyika  Dodoma chini ya udhamini wa Bank ya Azania na Qatar Airways kwa kumpatia Tiketi ya Ndege daraja la bishara (Business Class) kwenda Nchi yoyote Duniani atakayoichagua kwa ajili ya Mapumziko kwa siku atakazochagua yeye.

Mhe. Esther Nicholas Matiko ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu kutokea Mkoa wa Mara ambaye na Shabiki wa Timu ya Simba ameibuka kidedea kwa kujinyakulia Medali za Dhahabu Tatu (3) akiwakilisha Mashabiki wa Timu ya Simba Sc kwa kuwashinda washindani wake ambao ni Mashabiki wa Timu ya Yanga.

Kumalizika kwa Bonanza hilo lililojumuhisha michezo mbalimbali ikiwa ni michezo ya mtu mmoja mmoja na ile inayojumuhisha muunganiko wa Timu, Mhe Esther Nicholas Matiko amekuwa Mchezaji pekee aliyejinyakulia Medali nyingi zaidi ya wachezaji wengine zipatazo 7 (Medali 3 binafsi na Medali 4 za Timu) katika Bonanza hilo lililofanyika 27/01/2024 chino ya udhamini na Bank ya Azania.

Mhe. Esther Nicholas Matiko ameibuka mshindi katika michezo ya Karata Wanawake, Pull Table Wanawake, Mchezo wa Bao Wanawake na upande wa Timu ameshinda Mpira wa Pete, Mpira wa Wavu, Mpira wa Kikapu na Riadha mita 100

Mhe. Esther Nicholas Matiko ameendelea kung’ara katika mashindano mbalimbali yanayojumuhisha Wabunge wa Tanzania na hata yale mashindano ya Mabunge Afrika ya Mashariki.

Chapisha Maoni

0 Maoni