Jamii imetakiwa kuzingatia mtindo bora wa maisha na kufuata
ulaji sahihi kama wanavyoshauriwa na wataalam wa afya ili kujikinga na magonjwa
yasiyoambukiza ikiwemo magonjwa ya figo.
Hayo yamesema leo na Dkt.Gunini Kamba, akizungumza kwa niaba
ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam ambaye alikua mgeni rasmi katika hafla
fupi ya kukabidhi tuzo na medali kwa baadhi ya watumishi wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili na taasisi nyingine zilizotolewa na Taasisi ya Profesa Jay ikiwa ni
kutambua mchango wao katika kutoa huduma za afya.
Dr. Kamba amesema magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo magonjwa
ya figo yanazidi kuongezeka na gharama
za matibabu kwa magonjwa hayo ni kubwa
na si kila mwananchi anayeweza kumudu gharama hizo hivyo ni vyema jamii
ikatambua hilo ili iweze kujikingwa kwa kuwa king ani bora kuliko tiba.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya
Wadhamini Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Ellen Senkoro ameipongeza Taasisi
ya Professor Jay kwa kutambua mchango mkubwa unaofanywa na Hospitali ya
Muhimbili na kuwapongeza baadhi ya watumishi ambao wamechaguliwa kupata tuzo
hizo na kusema kuwa Muhimbili itaendelea kutoa mchango kwa tasisi hiyo ili
indelee kutoa hamasa kwa jamii kuhusu afya.
“Hili ni jambo la kiubunifu ambalo taasisi ya Professor Jay
imefanya kwani halijawahi kutokea, pia niwapongeze watumishi wote ambao
mmepatiwa tuzo najua nyie ni wawakilishi wa baadhi ya watuishi takribani 3000
ambao mnafanya kazi kwa kujituma, ” amesema Dkt. Senkoro.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili Prof. Mohamed Janabi amesema kuwa kwa siku MNH-Upanga inatoa huduma
ya kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo 120 hadi 130 ambapo asilimia 90 ya
magonjwa wa hayo yanasababishwa ya shinikizo la juu la damu pamoja na kisukari
ambapo chanzo chake nikutozingatia lishe sahihi hivyo ni vyema watu
wakazingatia swala la lishe bora.
Awali akizungumza baada ya kukabidhi tuzo hizo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Professor Jay Florian Rutabingwa amesema taasisi hiyo itaendelea kutoa elimu ya afya kwa jamii ili kusaidia jamii kujikinga na magonjwa hayo ambayo yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku.
0 Maoni