Matukio mbalimbali ziara ya Rais Samia nchini Norway

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkuu wa Chuo Kikuu cha Oslo Profesa Svein Stølen wakati akimuelezea kuhusu masuala ya Tabianchi katika Jengo la Climate, Oslo Nchini Norway tarehe 14 Februari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia magome ya miti ambayo yamehifadhiwa katika Jengo la Climate, Oslo Nchini Norway tarehe 14 Februari, 2024.

Wageni mbalimbali pamoja na baadhi ya viongozi wakiwa kwenye mkutano wa Kilimo na Usalama wa Chakula uliofanyika katika Jengo la Climate, Oslo Nchini Norway tarehe 14 Februari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika mkutano wa Kilimo na Usalama wa Chakula uliofanyika katika Jengo la Climate, Oslo Nchini Norway tarehe 14 Februari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkuu wa Chuo Kikuu cha Oslo Profesa Svein Stølen wakati akimuelezea Mnyama aina ya Dubu (Bear) katika jengo la Climate House iliyopo Jijini Oslo Nchini Norway tarehe 14 Februari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia Donge la Barafu na jinsi linavyoyeyuka kutokana na mabadiliko ya Tabianchi mara baada ya kuwasili katika jengo la Climate House Jijini Oslo Nchini Norway tarehe 14 Februari, 2024. Kushoto ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Oslo Profesa Svein Stølen akiwa pamoja na Mwanamfalme wa Haakon wa Norway.

Chapisha Maoni

0 Maoni