Vyama vya Siasa vyakumbushwa kufanya uchaguzi wa viongozi

 

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi amevitaka vyama vya siasa ambavyo muda wa uongozi wa viongozi wake unakaribia kuisha, kufanya uchaguzi wa viongozi wake kabla ya muda huo kuisha.

Taarifa ya iliyotolewa Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Sisty Nyahoza imesema mwaka huu wa 2024 kuna idadi kubwa ya vyama vya siasa ambavyo muda wa viongozi wake unaisha hivyo vinapaswa kufanya uchaguzi.

Kifungu cha 9(2)(e) kikisomwa pamoja na Kifungu cha 8D(1) cha Sheria ya "The Political Act, CAP 258 kinaeleza kuwa kila chama kinapaswa kufanya uchaguzi wa kidemokrasia wa viongozi wake kwa vipindi ambavyo vimewekwa katika Katiba yake, imesema taarifa hiyo.

Pia, Kanuni ya 16 ya "Political Parties (Registration and Monitoring) Regulations 2019 (TS. 953/2019)" inaeleza kuwa uchaguzi wa viongozi wa chama cha siasa unapaswa kufanyika sio zaidi ya miaka mitano tangu uchaguzi ulipota, na kwamba chama kitaomba ruhusa ya Msajili wa Vyama vya Siasa endapo kinataka kufanya uchaguzi zaidi ya kipindi hicho.

Chapisha Maoni

0 Maoni