Cuba kuimarisha ushirikiano katika sekta nne ikiwemo Utalii

 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) leo Januari 24, 2024 ameungana na viongozi wengine kushiriki kikao kati ya  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango na Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Mesa, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Cuba zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wa maendeleo katika sekta za kipaumbele ambazo ni Elimu, Afya, Kilimo na Utalii.

Awali viongozi hao walishuhudia utiaji saini wa Hati mbili za Makubaliano ya Ushirikiano (MoUs) ambazo ni makubaliano kati ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na Chuo Kikuu cha Artimesa Diaz Gonzalez cha Cuba.

Hati ya pili ya Makubaliano ni kati ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) na Kituo cha Afya cha Taifa cha Udhibiti na Vifaa Tiba (CECMED) cha Serikali ya Cuba kwa lengo la kupanua wigo katika na kuongeza matumizi ya teknolojia katika masuala ya dawa na vifaa tiba.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) kulia, akiwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu wakifuatilia kwa makini kikao kati ya  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango na Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Mesa, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

 


Chapisha Maoni

0 Maoni