Wakristo wa Ukraine wa Orthodox wanasherehekea kwa mara ya kwanza Sikukuu ya Krismasi Desemba 25 katika mwaka huu.
Kwa utamaduni, Ukraine ilikuwa ikiitumia kalenda ya Julian
ambayo pia hutumika nchini Urusi, ambayo siku ya Krismasi huwa ni Januari 7.
Katika kuonyesha kuachana na Urusi, sasa Ukraine imeaamua
kuadhimisha Krismasi na mataifa ya magharibi kwa kutumia kalenda ya Gregorian
inayotumika katika maisha ya kila siku.
Mwezi Julai, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alibadilisha
sheria, na kuwafanya wananchi wa Ukraine kuachana na tamaduni za Urusi za
kusherehekea Krismasi Januari.
0 Maoni