Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
Geophrey Pinda amesheherekea Sikukuu ya Krismasi akiwa katika jimbo lake la
Kavuu lililopo wilaya ya Mlele mkoani Katavi.
Akiwa jomboni humo, Naibu Waziri Pinda alishiriki ibada ya Krismasi katika Kanisa Katoliki
Parokia Teule ya Bikira Malia Mpalizwa Mbinguni Kibaoni ambako alishiriki pia
harambee ya ya ujenzi wa nyumba za mapadri wa kanisa hilo na kuahidi kuchangia mifuko 200 ya Saruji. Ujenzi wa
nyumba hizo utagharimu shilingi milioni 75.
Ibada hiyo ya Krismasi katika kanisa hilo ilihudhuriwa pia
na kaka yake Mhe. Pinda ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Kayanza Peter
Pinda.
Aidha, Naibu Waziri Pinda akiwa eneo la Kibaoni ambapo ndipo
yalipo makazi yake wilayani Mlele mkoani Katavi alijumuika na baadhi ya wananchi wa eneo hilo wakiwemo viongozi wa
Chama cha Mapinduzi wilaya ya Mlele katika kusheherekea siku hiyo ya
Noeli.
Naibu Waziri Pinda yuko jimboni kwake katika jimbo la Kavuu wilayani Mlele mkoa wa Katavi pamoja na mambo mengine kujumuika na wapiga kura wake kutafakari utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika jimbo hilo.
Na. Munir Shemweta- WANMM Mlele
0 Maoni