Shirika la Afya Duniani
(WHO) limesema kwamba hospitali kubwa ya Gaza ya Al-Shifa inakaribia kuwa “eneo
la makaburi” kutokana na miili ya watu kujaa ndani na nje.
Makumi ya watoto njiti na
wagonjwa 45 wa figo wanaohitaji kufanyiwa dialysis hawawezi kutibiwa kwa
usahihi kutokana na kukosekana kwa umeme, Msemaji wa UN amesema.
Mapigano yamekuwa
yakishamiri karibu na hospitali kwenye Jiji la Gaza katika siku za hivi
karibuni, huku uhaba mkubwa wa mafuta ukiathiri matibabu.
Israel imekuwa ikiwatuhumu
Hamas kwa kutumia hospitali kuanzisha mashambulizi yao, huku hospitali hiyo na
Hamas wakikanusha madai hayo.
Israel ilianza kushambulia
Gaza, baada ya Hamas kufanya shambulizi Oktoba 7, ambalo liliua watu 1,200 na
zaidi ya 200 wakipelekwa hospitali.
0 Maoni