Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
TAMISEMI Mhe Mohamed Mchengerwa akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Mhe Albert Chalamila ametembelea na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Soko
la Kisasa la Kariakoo ambapo amesema ameridhishwa na maendeleo ya Ujenzi huo.
Amemshukuru Mhe Rais Dkt
Samia kwa kutoa pesa ambazo zinawezesha utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa
kisasa ambao kukamilika kwake utafungua fursa nyingi pamoja na kuchukua wafanyabishara
wengi zaidi tofauti na ilivyokua awali.
Aidha, Mhe. Mchengerwa amemtaka
mkandarasi kuendelea kujenga katika kiwango stahiki, kuzingatia ubora na
thamani ya pesa, pia amesema Soko likikamilika atamuomba Mhe Rais aje
kulifungua rasmi.
Vilevile Mhe Albert Chalamila
amemshukuru Rais Dkt Samia na Waziri wa OR-TAMISENI ambapo amesema amepokea
maelekezo yake yatafanyiwa kazi kwa wakati, pia amemhakikishia kuendelea
kumlipa mkandarasi pesa kwa wakati hata hivyo ametoa tahadhari kwa wananchi
kuepuka matapeli hadi sasa hakuna chumba kilichopangishwa muda ukifika
utaratibu utakuwa wazi lakini kikubwa wananchi wajue uwekezaji uliofanyika ni
mkubwa hivyo hata Kodi zitapitiwa tena ili ziendane na uhalisia.
Hata hivyo amewataka watakao
pata fursa ya kufanya biashara katika Soko hilo kulipa Kodi na sio kukwepa
kodi, amesistiza kwa kutambua umuhimu wa Kariakoo Serikali inaendelea
Kuimarisha Ulinzi na Usalama ili watu wafanye biashara saa 24 pia mifumo ya
CCTV camera itafungwa.
0 Maoni