Rais William Ruto wa Kenya amepiga marufuku kuingiza mazao
ya nafaka ya mahindi na ngano kutoka nje ya nchi ili kulinda soko la ndani
dhidi ya mazao yanayoingizwa nchini humo na kuuzwa bei nafuu hali inayoathiri
bei za nafaka.
Rais Ruto amesitisha utoaji vibali vipya vya kuagiza nafaka
kutoka nje ya nchi, na kusema kwamba Serikali yake itabadili msimamo wake huo
pale tu itakapobainika nchi inakabiliwa na uhaba wa nafaka.
Pia, amebainisha kwamba Serikali ya Kenya imetenga shilingi
bilioni 4 za nchi hiyo kwa ajili ya kununua mahindi kutoka kwa wakulima ambao
wameshaanza kuvuna mazao yao, kabla ya kuanza mvua za El Nino.
Agizo hilo la Ruto, litaziathiri baadhi ya nchi za Afrika
Mashariki ambazo zimekuwa zikiiuzia Kenya mazao ya nafaka hususan mahindi,
ambapo Tanzania na Uganda ni mingoni mwa nchi ambazo hunufaika na soko la mazao
la Kenya.
CHANZO: Nation
0 Maoni