Algeria yahaha kudhibiti kunguni wa Ufaransa wasiingie

 

Mamlaka za afya nchini Algeria, zimeimarisha hatua za kudhibiti mipaka kuzuia kusambaa kwa kunguni, ambao wametapakaa nchi ya Ufaransa.

Wizara ya Afya ya Taifa hilo la Kaskazini mwa Afrika, imesema imekuwa ikichukua hatua za kunyunyizia dawa za kulia wadudu kwenye ndege, meli na magari yanayoingia nchini humo.

Hatua hizo zinakuja baada ya wadudu hao wanafyonza damu kuwa na uwezekano wa kuingia Algeria kutokana na idadi kubwa ya watu wanaosafiri kutoka Ufaransa.

Hata hivyo wizara hiyo imesema, hakuna kunguni waliongia Algeria kutoka Ufaransa, na kuhimiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari.

Nchi ya jirani ya Morocco nayo tayari imeshatangaza hatua za kuzuia hatari ya kuingia kunguni hao kutoka Ufaransa.

Chapisha Maoni

0 Maoni