RC Chalamila ajionea uwekezaji hospitali ya Aga Khan

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Oktoba 5, 2023 ametembelea Hospitali ya Aga Khan - Tanzania kujionea namna hospitali hiyo inavyotoa huduma za afya kwa jamii, ikitumia vifaa tiba vya teknolojia ya kisasa.

RC Chalamila akiwa Hospitalini hapo ametembelea maeneo mbalimbali yenye vifaa tiba vya kisasa vinavyotumia teknolojia ya hali ya juu ya utoaji huduma za Afya pia amejionea Ujenzi wa jengo maalum litakalo toa huduma za kutibu magonjwa ya Cansa.

Vilevile Mhe Albert Chalamila amepongeza kazi nzurii inayofanywa ya kupambana na adui maradhi ambayo inamatokeo ya moja kwa moja kwenye kukuza na kuimarisha uchumi na maendeleo ya nchi ambayo ndiyo dhamira ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Watanzania, pia amefurahishwa na miundo mbinu ya hospitali hiyo, wataalam wenye uwezo mkubwa, usafi wa mandhari na mapangilio wa vitu.

Aidha, Mkuu wa Mkoa ameutaka uongozi wa hospitali hiyo kuwa uhuishaji wa taaluma za watumishi iwe ni tabia isiyo na kikomo, vilevile kusimamia vizuri upatikanaji wa huduma kwa gharama ambayo watu wengi wanaweza kumudu.

Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam Tanzania Sisawo Konteh amesema wamekua wakipata ushirikiano mkubwa kutoka serikarini na amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa Aga Khan itaendelea kuwekeza Dar es Salaam kwa masilahi mapana ya Umma.

Mwisho Mhe Albert Chalamila katika ziara yake ameambatana na Katibu Tawala wa Mkoa Bi Rehema Madenge, wataalam kutoka Idara ya Afya, DAWASA, TANESCO, na TRA.

Chapisha Maoni

0 Maoni