Waliokufa kwa mafuriko Libya wazikwa makaburi ya pamoja

 

Miili ya watu iliyopatikana katika eneo lililokumbwa na mafuriko mashariki mwa Libya imezikwa katika makaburi ya pamoja.

Watu wapatao 2,300 wamekufa, huku 10,000 hawajulikani walipo, baada ya mafuriko makubwa mithili ya mto kusomba sehemu ya mji wa Derna.

Waokoaji wanachimba kwenye vifusi kutafuta miili ya watu waliofukiwa baada ya kutokea kwa mafuriko hayo siku ya jumapili.

Umoja wa Mataifa umesema kwamba maafa ya mafuriko hayo, yamewaathiri watu wanaokadiriwa kufikia milioni 1.8.

Wakati huo huo, waokoaji watatu wa kujitolea wamekufa wakati wakijaribu kuwaokoa watu walioathiriwa na mafuriko hayo.

Chapisha Maoni

0 Maoni