Kim aahidi kupigana na ubeberu akikutana na Putin

 

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na Rais Vladimir Putin wamekutana huko Voctochny eneo la mashariki mwa Urusi.

Kim amemuambia Putin kwamba atamuunga mkono daima na kwa pamoja watapambana na ubeberu.

Kwa upande wake Putin amesema kwamba Urusi itaisaidia Korea Kaskazini kujenga satelaiti, baada ya taifa hilo kushindwa mara mbili mwaka huu kurusha satelaiti.

Inahofiwa kuwa viongozi hao wawili pia wanaweza wakakamilisha makubaliano ya kuisaidia silaha Urusi iliyoivamia Ukraine.

Alipoulizwa kuhusina na makubaliano ya masuala ya kijeshi, Rais Putin alisema kwamba watajadiliana kuhusina na suala hilo.

Kabla ya mkutano wao huo, Korea Kaskazini ilirusha makombora mawili, ikiwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo wakati Kim akiwa nje ya nchi.

Chapisha Maoni

0 Maoni