Serikali kinzani Libya zaratibu misaada ya mafuriko

 

Umoja wa Mataifa umesema Serikali mbili kinzani za Libya zimeweka kando tofauti zao na kuratibu jitihada za kupatikana misaada kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa.

Zaidi ya watu 5,300 wamekufa baada ya mabawa mawili kupasuka na kusababisha mafuriko yenye maafa makubwa mashariki mwa mji wa Derna.

Watu wapatao 10,000 hawajulikani walipo, na makumi kwa maelfu ya watu wamejikuta wakikosa makazi.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesema serikali zote za upande wa mashariki na magharibi pamoja na mataifa ya magharibi wameomba msaada kwa jumuia ya kimataifa.

Chapisha Maoni

0 Maoni