Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan
Abbasi, akiwa nchini Saudia Arabia katika Mkutano wa 45 wa Kamati ya Urithi wa
Dunia leo Septemba 13, 2023, amepata fursa ya kuongoza majadiliano kati ya
Tanzania na Uganda.
Majadiliano hayo yanahusu juu ya kushirikiana katika
kuainisha na kutangaza maeneo yenye michoro ya miambani iliyopo ukanda wa Ziwa
Victoria kwa nchi za Uganda, Tanzania na Kenya ili kuyaingiza kwa pamoja katika
Orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO.
Kufuatia mazungumzo hayo Katibu Mkuu ameelekeza watalaam wa
Idara ya Mambo ya Kale nchini waharakishe zoezi la kuainisha maeneo hayo ya Malikale
upande wa Tanzania ili yatangazwe na amewashukuru maafisa wa Africa World
Heritage Fund ambao wameeleza kusaidia nchi hizo tatu kufanikisha azma hiyo.
0 Maoni