Mtuhumiwa wa ugaidi atoroka gerezani London

 

Msako wa kitaifa umeanzishwa kumtafuta mtuhumiwa wa makossa ya ugaidi aliyewahi kuwa mwanajeshi, ambaye ametoroka gerezani Jumatano asubuhi.

Mtuhumiwa huyo Daniel Abed Khalife, 21, alikuwa anangojea kusikilizwa kesi zake HMP Wandsworth, Jijini London baada ya kutuhumiwa kuacha mabomu feki kwenye kambi ya jeshi.

Inaaminika kwamba mfungwa huyo alitoroka kupitia jiko la gereza kwa kujificha chini ya gari la kusambaza vyakula.

Ulinzi wa ziada umeimarishwa kwenye viwanja vya ndege na kwenye bandari na kusababisha kuchelewesha usafiri kwa muda mrefu.

Chapisha Maoni

0 Maoni