Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amewataka watendaji wake kushirikiana
kwa pamoja ili wananchi wapate huduma kwa wakati.
Waziri Ndalichako ameyasema hayo wakati wa kikao kazi cha
kujadili kazi za Ofisi hiyo pamoja na Taasisi zilizopo chini yake
kilichofanyika Septemba 6, 2023 katika jengo la OSHA jijini Dodoma.
Aidha Prof. Ndalichako ameongeza kuwa kila mtendaji
anajukumu la kutekeleza maagizo ya viongozi kwa haraka ili kuiwezesha serikali
kufikia malengo na kuleta tija kwa wananchi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja amemuhakikishia Waziri
Ndalichako kuwa majukumu ya ofisi hiyo yatatekelezwa kwa kuzingatia Sheria,
Taratibu na Kanuni.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)
Dkt. John Mduma akiongea kwa niaba ya Wakurugenzi Watendaji wa Taasisi zilizo
chini ya Ofisi hiyo, amebainisha kuwa wataendelea kutoa ushirikiano kwa Katibu
Mkuu huyo mpya ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya wizara pamoja na
taasisi zake.
0 Maoni