Askofu Mkuu Novatus Rugambwa, Mtanzania ambaye aliwahi kuwa Balozi wa Baba Mtakatifu (Vatican) katika nchi mbalimbali duniani, amefariki dunia usiku wa Septemba 16, 2025 jijini Roma, nchini Italia.
Marehemu Askofu Mkuu Rugambwa alizaliwa Oktoba 8, 1957, mkoani Kagera, na aliwekwa wakfu kuwa Padre tarehe 6 Julai, 1986 na aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Mhashamu Nestorius Timanywa.
Baadaye, Machi 18, 2010, aliwekwa wakfu kuwa Askofu na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Vatican, Askofu Mkuu Tarcisio Pietro Evasio Kardinali Bertone.
Katika maisha yake ya kiutumishi, Askofu Mkuu Rugambwa aliwakilisha Vatican kama Balozi wa Papa katika mataifa mbalimbali ikiwemo Angola, Honduras, na Visiwa vya Fiji, miongoni mwa mengine.
Waumini wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania na duniani kwa ujumla wanamkumbuka kama mtumishi mwaminifu aliyejitolea maisha yake kuhudumia Kanisa na kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya Vatican na nchi mbalimbali.
"Raha ya milele umpe Ee Bwana, na mwanga wa milele umwangazie. Apumzike kwa amani."
Amina.
0 Maoni