Idara ya Usalama na Intelejensia ya Burkina Faso imezima
jaribio la mapinduzi Jumanne, kwa mujibu wa Serikali ya kijeshi ya nchi hiyo.
Imedaiwa kuwa baadhi ya maafisa wa jeshi na watu wengine
walipanga kutibua hali ya usalama wa nchi hiyo na kuitumbukiza kwenye
machafuko.
Tukio hilo limetokea ikiwa ni chini ya mwaka mmoja, tangu
rais wa mpito wa nchi hiyo Kapteni Ibrahim Traore atwae madaraka kwa njia ya
mapinduzi.
Taarifa iliyosomwa kupitia televisheni, imeeleza mamlaka ya
Burkina Faso imewakamata baadhi ya wahusikawa jaribio la mapinduzi, bila ya
kutoa taarifa zaidi.
0 Maoni