Wananchi wa Zimbabwe kupiga kura ya kumchagua rais wao leo

 

Nchi ya Zimbabwe leo inaelekea kwenye uchaguzi wa rais na uchaguzi wa serikali za mitaa, baada ya kumalizika kwa kampeni zilizotawaliwa na suala la mfumuko wa bei.

Siku ya uchaguzi wa Zimbabwe imetangazwa kuwa ni siku ya mapumziko ili kutoa fursa wapiga kura milioni 6.62 kushiriki kupiga kura.

Rais Emmerson Mnangagwa anakabiliwa na wagombea urais 10, akiwamo Nelson Chamisa wa chama kikuu cha Citizens Coalition for Change (CCC).

Mshindi wa urais anapaswa kupata kura zaidi ya asilimia 50 ya kura zote, iwapo hatopata kura hizo uchaguzi utarudia ndani ya wiki sita Oktoba 2.

Chapisha Maoni

0 Maoni