Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Luteni
Kanali Frederick Faustine Komba ametoa wito kwa vijana waliohitimu mafunzo ya
kwa mujibu wa sheria Operesheni Nishati Safi 2025 kutomezwa na mitandao ya
kijamii kwa sababu imekua chanzo cha kupoteza maadili .
DC Rufiji Luteni Kanali Komba amesema hayo wakati
alipokua mgeni rasmi kwenye sherehe za kufunga
mafunzo ya Oparesheni Nishati Safi
katika Kikosi 830 Kibiti Mkoani
Pwani.
"Zamani kulikua na
sherehe za jando kwa wanaume na
unyago kwa mabinti ambao walifindwa
namna ya kuishi vizuri katika jamii hivyo basi mafunzo haya kwa vijana
yanayotolewa na Jeshi la Kujenga Taifa
(JKT) yamebeba maudhui hayohayo ya
kuwafundisha vijana namna ya kuishi vema
katika jamii.
Akifunga mafunzo hayo ya Operesheni
Nishati Safi Luteni Kanali Komba ametoa
pongezi kwa Mkuu wa Kikosi cha Kibiti
830 Mohammed Karuma pamoja na wakufunzi wote kutokana na mafunzo
waliyoyatoa kwa vijana hao.
"Natoa pongezi zangu za
dhati kwa Mkuu wa Kikosi Kanali Mohammed
Karuma pamoja na wakufunzi wote kwa
ujumla kutokana na mafunzo waliyoyatoa kwa vijana hawa ambao wametoka katika
Mikoa mbalimbali mbalimbali nchini mwetu
huku wote wamekua wamoja" amesema Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Luteni Kanali
Komba.
Amesema kuwa weledi wa wakufunzi
hao umewabadilisha vijana hao na kuwa wamoja na kuwasisitiza wahitimu hao
waende kuishi waliyofundishwa.
"Nendeni mkawe mabalozi
wazuri wa mafunzo ya JKT huko muendako
mkawe wawakilishi wema pia mtambue
kwamba maisha siyo rahisi mkajitunze na kuwa timamu kitabia na kiafya sababu ninyi ndiyo viongozi wa taifa
letu kesho" amesema DC Rufiji Luteni Kanali Komba.
Wakati huo huo amewataka vijana
waliohitimu Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT kwa Mujibu wa sheria 2025 kulinda kiapo chao na
kutenda yale waliyofundishwa pindi watakaporejea nyumbani.
Yamesemwa hayo
na aliyekuwa mgeni rasmi katika kufunga mafunzo kwenye sherehe
iliyifanyika tarehe 18 Septemba
2025,yanayofahamika kama Operesheni
Nishati safi katika kikosi 830 Kibiti kilichopo Mkoani Pwani.
Naye Mkurugenzi Rasilimali Watu
Makao Makuu ya Jeshi Brigedia Jenerali Simon Pigapiga kwa Niaba ya Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Jacob Mkunda amewataka vijana wanaohitimu
mafunzo hayo kutumia kwa faida ujuzi waliyo upata katika kipindi chote cha
mafunzo yao.
Aidha, Kanali Aranyael Nnko
ambaye ni mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu
Mabele amesema mafunzo hayo yamefanyika kwa kipindi cha majuma kumi na Mawili yakijumuisha mafunzo ya
awali ya kijeshi, Kazi za mikono na
uzalishaji Mali.
Wakati huohuo ametoa shukrani kwa
wazazi waliotoa fursa kwa vijana wao kuhudhuria
mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria 2025 ambayo
kimsingi yanamjengea Kijana Uzalendo na Moyo wa Kupenda kazi.
"JKT ni mahali sahihi na salama hivyo jamii na wazazi msisite kuleta vijana wenu kuja kupata nafasi
hii ambayo huwasaidia kuwajenga kizalendo na kuwapa mafunzo ya awali ya ulinzi
na usalama pia ni haki kwa vijana wa kitanzania katika Kufundishwa Uzalendo na
siyo vinginevyo" amesema Luteni Kanali Komba.
0 Maoni