NBA yampiga faini ya dola laki moja James Harded

 

James Harden amepigwa faini ya dola 100,000 na NBA kwa kusema kuwa hatoichezea Philadelphia76ers, iwapo rais Daryl Morey ataendelea kuwapo madarakani.

Mchezaji huyo wa ligi ya NBA, alimuita Morey “muongo” kwenye mahojiano baada ya ripoti kuwa 76ers imesitisha mazungumzo ya kumuuza.

Harden, mwenye umri wa miaka 33, aliripotiwa kutamani kujiunga na timu ya LA Clippers kabla ya mazungumzo ya mpango huo kuzimwa.

NBA imesema kuwa faini hiyo ni kwa kusema hatotekeleza majukumu yake ya kuichezea timu hiyo iwapo hatouzwa timu nyingine kinyume na mkataba wake wa kazi.

Chapisha Maoni

0 Maoni