Rais Samia Suluhu Hassan akibadilishana mawazo na Rais wa
Brazil, Lula Da Silva pamoja na Waziri wa mambo ya nje wa Urusi muda huu baada
ya kukamilika kwa mkutano wa kumi na tano wa Jumuiya ya BRICS.
BRICS ni Jumuiya kubwa ya pili kiuchumi duniani,
ikiwakilisha idadi ya watu wanaokaribia bilioni 3.5 inaundwa na nchi za Urusi,
China, Brazil, Afrika ya Kusini na India.
Saudi Arabia, Egypt, UAE, Argentina, Iran na Ethiopia
watakuwa ni wanachama wapya kuanzia january Mosi, 2024
Asilimia 80 ya uzalishaji wa mafuta unatoka katika nchi
zinazounda umoja wa BRICS.
0 Maoni