Malima Masota anayedaiwa kuendesha gari kwa mwendo kasi na
kusababisha kifo cha mwanafunzi Consolatha Marwa ameangua kilio mahakamani
baada ya kukosa dhamana kwa kushindwa kutimiza masharti.
Dereva huyo amesomewa mashtaka yanayomkabili likiwemo la
kuendesha gari kwa kwendo kasi na kusababisha kifo cha mwanafunzi huyo aitwaye
Consolatha kinyume na kifungu namba 40, 63 (2) (a) naa 26 (1) (a)cha sheria ya
usalama barabarani namba 168 marejeo ya mwaka 2002 na kumjeruhi mwanafunzi
mwingine aitwaye Magreth Ntemi pamoja na kuendwsha gari isiyokuwa na bima
kinyume na kifungu namba 4(1) na 2 cha sheria ya bima ya magari namba 169
marejeo 2002.
Mmiliki wa gari hilo lenye namba za usajili T. 121 DCU,
Athuman Mussa ameangua kilio katika mahakama ya wilaya ya Magu baada ya
kushindwa kutumiza masharti ya dhamana ambapo dereva na mmliki wa gari hilo
walifunguliwa kesi ya trafiki namba 19 ya mwaka huu ambayo imesomwa mbele ya Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Amon Rwegoshora
Baada ya kusomewa mashtaka mshtakiwa namba moja, amekidhi
masharti ya dhamana ambayo ni kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika
watakaosaini bondi ya maneno ya sh milioni 4 kila mmoja huku mshtakiwa namba
mbili akishindwa kukidhi masharti hayo kutokana na kuwa na mdhamini mmoja na
kurudishwa rumande katika gereza la wilaya ya Magu.
Mwendesha Mashtaka, Ilole amesema upelelezi wa kesi hiyo
umekamilika, huku Hakimu, Rwegoshora akiahirisha kesi hiyo hadi Agosti 31,
mwaka huu itakapotajwa kwa ajili ya washtakiwa kuanza kusomewa maelezo ya
awali.
Ajali hiyo ilitokea Agosti 11, 2023 majira ya saa saba
mchana katika mtaa wa Nyalikungu "A" wilayani Magu mkoa wa Mwanza
iliyohusisha gari yenye namba za usajili T.121 DCU aina ya Toyota Hiace ambapo dereva
wa gari hiyo alitoroka baada ya ajali na baadae kukamatwa na jeshi la polisi.
Kupitia taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari Agosti 12
mwaka huu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza SACP Wilbrod Mutafungwa alisema
ajali hiyo iliyotokea katika mtaa wa Nyalikungu 'A' wilayani Magu, kwa gari
hilo kuwagonga wanafunzi waliokuwa wakivuka barabara na kusababisha kifo cha
mwanafunzi mmoja na kujeruhi mwingine.
0 Maoni