Trump kujisalimisha Mahakamani Georgia siku ya Alhamisi

 

Donald Trump amesema anapanga kujisalimisha Mahakamani siku ya Alhamisi katika jimbo la Georgia kukabiliana na mashtaka ya kuingilia uchaguzi.

Jaji wa Mahakama ya Atlanta anayesimamia kesi ya rais huyo wa zamani wa Marekani, amempangia kulipa dhamana ya dola 200,000 za Marekani.

Makubaliano ya kesi hiyo yanasema kwamba Trump ataendelea kuwa huru, iwapo tu hatojaribu kuwatisha mashahidi wa kesi hiyo.

Chapisha Maoni

0 Maoni