Kimbunga Hilary chaua mwanaume mmoja California

 

Kimbunga Hilary kimepungua nguvu kikielekea pwani ya Pacific ya Mexico na California lakini bado kinaweza kuhatarisha maisha kwa mafuriko, Watalamu wa Hali ya Hewa wa Marekani wamesema.

Kimbunga hicho chenye upepe wenye kasi ya kilomita 140 kwa saa, kimeshushwa kiwango chake cha madhara na kuwa cha daraja la kwanza.

Mwanaume mmoja amekufa huko California baada ya gari alilokuwa akiendesha kusombwa na maji, lakini watoto wake watatu na mkewe waliokuwamo wamenusurika kifo.

Chapisha Maoni

0 Maoni